Compass Communications. Co LTD, Inapenda kuutaarifu umma ya kuwa kuna genge la watu wanaotumia jina la mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa kijamii wa Facebook ili kuwarubuni wasichana.
Kuna ukurasa ujulikanao kama Flaviana Matata’s hutumika kama moja ya ukurasa wa Mwanamitindo huyu kitu ambacho si kweli. Watu hawa huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Mwanamitindo huyu.
Genge
hili la uhalifu hudai kuwa kuna ‘kaka’ yake Flaviana ambaye hukutana na
wasichana hawa na baada ya mazungumzo anawalaghai kwa njia mablimbali. Pia
wahusika hawa hutoza kiasi cha pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000
) kama tozo kwa huduma hii ya kuwatafutia
kazi nje ya nchi.
Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa. Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uanamitindo popote pale.
Ukurasa
halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata”. Hivi sasa
tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huu
na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Compass Communications. Co. LTD
No comments:
Post a Comment