Tuesday, April 9, 2013

MISS UNIVERSE TANZANIA KUANZA MSIMU MPYA WA 2013


Miss Universe Tanzania, chini ya kampuni ya Compass Communications siku ya tarehe 08/04/2013 wamefanya kikao cha Tathmini ikishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Akiongea mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai, amesema mbali na changamoto zote wanazokabiliana nazo lakini pia wameendelea kuboresha mashindano haya ikiwemo kuongeza mikoa ambapo sasa itafika mikoa 14 badala ya mikoa saba ya mwanzoni. Mikoa hiyo ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha, Mtwara, Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na Manyara.

Miss Universe Tanzania 2010, Hellen Deusen akimkabidhi taji Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu.
Washindi wa watatu wa Miss Universe Tanzania 2012.

 Vilevile Miss Universe Tanzania inapanga mikakati ya kuwaendeleza ya kuwasaidia wale ambao hawajashika nafasi za juu hususani wale waliokwama kielimu kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za hapa nchini hususani zinazoshughulika na masuala ya wanawake.
Vile Baraza la Sanaa Tanzania wametoa pongezi kwa waandaaji wa mashindano haya na kuwaasa waendelee na ubora huo ikiwemo kushughulikia changamoto ndogondogo zinazojitokeza.

 Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu na Miss Universe Tanzania 2012, Winfrida Dominic 
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu
Washindi wa watatu wa Miss Universe Tanzania 2011.

No comments:

Post a Comment