Miss Universe Tanzania, chini ya kampuni ya Compass
Communications siku ya tarehe 08/04/2013 wamefanya kikao cha Tathmini ikishirikisha wadau mbalimbali
ikiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Akiongea mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia
ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai, amesema mbali na
changamoto zote wanazokabiliana nazo lakini pia wameendelea kuboresha
mashindano haya ikiwemo kuongeza mikoa ambapo sasa itafika mikoa 14 badala ya
mikoa saba ya mwanzoni. Mikoa hiyo ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe,
Ruvuma, Dodoma, Arusha, Mtwara, Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na
Manyara.
|
Miss Universe Tanzania 2010, Hellen Deusen akimkabidhi taji Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu. |
|
Washindi wa watatu wa Miss Universe Tanzania 2012. |
Vilevile Miss Universe Tanzania inapanga mikakati ya
kuwaendeleza ya kuwasaidia wale ambao hawajashika nafasi za juu hususani wale
waliokwama kielimu kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za hapa nchini hususani
zinazoshughulika na masuala ya wanawake.
Vile Baraza la Sanaa Tanzania wametoa pongezi kwa waandaaji
wa mashindano haya na kuwaasa waendelee na ubora huo ikiwemo kushughulikia
changamoto ndogondogo zinazojitokeza.
|
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu na Miss Universe Tanzania 2012, Winfrida Dominic |
|
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu |
|
Washindi wa watatu wa Miss Universe Tanzania 2011. |
No comments:
Post a Comment