Wise AD

Wise AD

Monday, July 1, 2013

Rais Obama atua nchini Tanzania salama

Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda huu katika ratiba yake ya mwisho wa ziara barani Afrika. Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi na kisiasa wanaeleza kuwa ziara ya Rais Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.


 Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.


Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi.........

No comments:

Post a Comment