Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications imeanza msimu mpya wa mashindano yake ya urembo ya MISS UNIVERSE TANZANIA 2013/2014. Jumla ya mikoa 8 itashiriki katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mwakilishi atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Universe mapema mwezi Novemba 9 katika mji
wa Moscow nchini Urusi. Mikoa hiyo nane ni pamoja na Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Miss Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake tarehe katikati ya mwezi Septemba katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert street jijini Dar
es Salaam.
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010. Baadae taji lilichukuliwa na Nelly
Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic.
Fomu za ushiriki wa shindano la Miss Universe Tanzania mwaka 2013/2014 zinapatikana; ARUSHA-0767628890, MBEYA-0767628890, MANYARA-0767628890, MTWARA-0658561514, DODOMA-0714583777, MWANZA-0715471412, DAR ES SALAAM- +255 22 21 82 405.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na MWANAKOMBO SALIM - 0714 44 11 65, SEIF KABELELE-0713302075.
Facebook: https://www.facebook.com/MissUniverseTanzania?fref=ts
P.O BOX 105133, DAR ES SALAAM, TANZANIA , TEL: +255 22 2182405
No comments:
Post a Comment