Wise AD

Wise AD

Tuesday, April 22, 2014

Mafuriko Dar es Salaam yaua 41, mvua zaendelea kunyesha

MAFURIKO yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25 vimethibitishwa. Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, eneo la Ilala vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili awaonekani. Kinondoni vifo ni saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo ni saba.

Sadiki alitaka uchunguzi wa polisi ufanyike kila familia zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo vya watu 14 vilivyotokana na mafuriko.

Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.

Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake na wakazi hao wa maeneo hatarishi.

Wakazi wa Dar es Salaam wakipita jana kwenye daraja la mto Msimbazi eneo la Jangwani lililoharibiwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini.

No comments:

Post a Comment