Wise AD

Wise AD

Monday, June 9, 2014

MTV MAMA 2014: Mafikizolo wabeba tuzo kubwa, orodha kamili ya washindi

Safari ndefu ya ya mchakato wa tuzo za MTV (MAMA2014) Ulioanza rasmi April 16 baada ya kutangazwa majina ya nominees na kuanza kupigiwa kura imefikia ukingoni June 8 ICC Arena, Durba Afrika Kusini.
Mafikizolo MTV_full
Kwa mujibu ya matokeo ya mchakato mzima, Tanzania hatubahatika kupata tuzo hata moja kati ya tuzo mbili alizokuwa anawania Diamond Platinumz (Best Male Artist na Best Collaboration).
Davido ndiye aliyebeba tuzo ya Best Male Artist na tuzo nyingine kubwa ya Artist of The Year. Na Tiwa Savage aliipeleka Nigeria tuzo ya Best Female.
Kundi la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ndilo lililonyakua tuzo kubwa zaidi usiku huo, tuzo ya Wimbo bora wa mwaka na wimbo wao maarufu wa Khona waliomshirikisha Uhuru. Pia likashinda tuzo ya kundi bora (Best Group).
Mafikizolo wanawania pia tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act.
Moja kati ya surprise zilizowavuta wengi ni pale D’Banj alipoungana na Trey Songz jukwaani.
Macho ya watanzania na nguvu kubwa inaelekezwa BET ambako Diamond anawania tuzo ana kila dalili ya kuwazidi wenzake.

Hii ni orodha ya washindi:
Song of The Year - Khona-Mafikizolo feat Uhuru
Best Collaboration - Y-tjukutja – Uhuru feat DJ Buckz,                                    Oskido, Professor, Yuri Da Cunha
Best Music Video - Clarence Peters (Nigeria)
Best Francophone - Toofan (Togo)
Artist of the Year - Davido (Skelewu)
Best Hip Hop - Sarkodie (Ghana)
Best Group - Mafikizolo
Best New Act - Stanley Enow (Cameroon)
Best Female Artist - Tiwa Savage (Nigeria)
Best Male Artist - Davido (Nigeria)
Best Altenative - Gangs of Ballet (South Africa)
*Transform Today Award- Clarence Peters

No comments:

Post a Comment